Siafu amwokoa Njiwa
Kholeka Mabeta
Wiehan de Jager

Ilikuwa siku yenye joto jingi.

1

Siafu Mdogo hakuwa amepata maji kwa siku nyingi.

2

Akawaza, "Ninahitaji tone moja tu la maji, hata kama litatoka kwenye jani."

3

Umande wote ulikuwa umekauka.

Hangepata hata tone moja la moja.

4

Siafu Mdogo akalia sana, "Nisipokunywa maji, nitakufa. Lazima niufikie mto nilioelezwa."

5

"Ati mtoni? Huko utakufa maji!" Kichakuro mmoja mwenye hekima alimwonya.

6

Lakini, Siafu Mdogo hakujali. Kiu chake kiliongezeka.

"Nitakufa iwapo sitakunywa maji sasa."

7

Siafu Mdogo alienda kuutafuta mto alioambiwa juu yake.

8

Alipitia kwenye nyasi na matawi yaliyokauka.

9

Mara akasikia mngurumo wa mawimbi.

10

Siafu Mdogo alifika mtoni akayanywa maji baridi.

11

Alifurahi kukata kiu na hakuliona wimbi kubwa likija.

12

Siafu Mdogo alijaribu kujishikilia kwenye nyasi kavu zilizokuwa zikielea.

Lakini, alisombwa na maji.

13

Siafu Mdogo alilia, "Jamani, nisaidieni."

14

Njiwa Mweupe alikuja akamnyooshea tawi. Akasema, "Panda juu ya tawi haraka."

15

Siafu Mdogo aliruka juu ya tawi na Njiwa Mweupe akamwokoa.

16

Siafu Mdogo akasema, "Siondoki kabla sijamshukuru Njiwa. Nitasubiri hadi atakaporejea kunywa maji."

17

Siku moja alipokuwa akimsubiri Njiwa Mweupe, Jona na Petro walikuja mtoni.

Walikuwa wamebeba manati.

18

"Yule Njiwa Mweupe ambaye huja hapa kunywa maji, tutamla jioni," Jona akawaza.

19

Jona na Petro walijificha nyuma ya mimea kando ya mto.

20

"Sitakubali wajanja hao wamuue yule Njiwa Mweupe. Lakini nitafanyaje? Mimi ni mdogo sana," Siafu aliwaza.

21

Wakati huo huo Njiwa Mweupe aliruka kutoka mtini anywe maji.

22

Jona na Petro walipima shabaha na kungoja kwa hamu.

23

Siafu Mdogo alipata wazo.

24

Aliurukia mguu wa Petro na kumuuma.

25

Petro aliruka juu akalia kwa uchungu, "Waaa!"

Aliyaachilia manati yake yakaanguka.

26

Njiwa Mweupe alishtuka akaondoka.

27

Hivyo ndivyo Siafu Mdogo alivyomwokoa Njiwa Mweupe.

28
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Siafu amwokoa Njiwa
Author - Kholeka Mabeta, Judith Baker
Translation - Ursula Nafula
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - First sentences