Yayeri anaamka mapema. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anashukuru kwa usiku uliopita. Tunauliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anatandika godoro vizuri. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anawasalimu babu na bibi. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anaosha uso wake. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anapiga meno yake mswaki. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anaoga. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anavaa sare ya shule. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anavaa viatu vyake vyeusi. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anafika shuleni mapema. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anasoma kwa bidii. Tunajiuliza, "Kwa nini Yayeri ni mashuhuri?"
Anacheza na wenzake. Unaelewa kwa nini Yayeri ni mashuhuri?