Mbweha na zabibu chachu
Kholeka Mabeta
Benjamin Mitchley

Hapo zamani za kale, palikuwa na Mbweha aliyekuwa na njaa.

Alitembea karibu na kichaka akitafuta chakula.

1

Aliuona mzabibu uliojaa zabibu mbivu.

Kichala cha zabibu mbivu kilining'inia.

2

Mbweha aliwaza, "Zabibu hizi zinaonekana tamu kweli kweli."

Alirudi nyuma hatua chache ili aweze kuzirukia zile zabibu.

3

Zabibu zilikuwa juu sana.

Mbweha alipozirukia, alianguka kwa mgongo wala hakuzifikia zile zabibu.

4

Aliinuka akurudi nyuma zaidi ili aweze kuzifikia zabibu.

Mara hii alifika karibu zaidi, lakini akaanguka tena kwa kishindo.

5

Alijaribu tena na tena, lakini hakuweza kuzifikia zabibu.

Alianguka mara nying hadi mgongo ukamuuma.

6

Hatimaye, alikata tamaa na kwenda zake.

7

Mbweha alijawa na majuto. Alisimama, akatazama nyuma na kuziangalia tena zile zabibu, "Zabibu hizo, hata hivyo, zinaonekana chachu." Akajiliwaza.

Aliondoka akaenda zake huku akihisi njaa kuliko hapo awali.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Mbweha na zabibu chachu
Author - Kholeka Mabeta
Translation - Brigid Simiyu
Illustration - Benjamin Mitchley
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs