Huyu ni ng'ombe mtulivu.
Mchana yeye ni ng'ombe wa kawaida.
Hupeperusha tiara.
Au kucheza mpira.
Usiku yeye hubadilika na kuwa Ng'ombe Shujaa.
Yeye huokoa maisha.
Na kupambana na uhalifu.
Wewe pia ukiyafumba macho yako kabisa, kisha uwe na hamu kubwa.
Huenda ng'ombe akakutembelea pia!