Banti na Sabuni
Sorit Gupto
Sorit Gupto

Banti anapenda kucheza na vipepeo.

1

Pia anapenda kucheza na ndege.

2

Yeye hutengeneza mashua kutoka kwa makaratasi.

3

Pia hutengeneza ngome akitumia changarawe.

4

Banti akirudi nyumbani, mamake humwuliza aoge.

Yeye hukataa.

5

"Nachukia sabuni!" Banti hulia.

6

Aliota kuwa viini vinavyosababisha magonjwa vilikivamia kitanda chake.

7

Banti alikuwa anafukuzwa na viini hivyo.

Alikimbia akipiga mayowe, "Nisaidieni. Nisaidieni!"

8

Mfalme Sabuni alimjibu, "Banti, usiogope. Jeshi langu la povu litavivamia viini vile vinavyokusumbua!"

9

Mara moja, povu lilivifukuzia mbali viini vile.

10

Tangu wakati huo, Banti hutumia sabuni.

Hujipangusa na kujisugua hadi huwa msafi.

11
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Banti na Sabuni
Author - Sorit Gupto
Translation - Brigid Simiyu
Illustration - Sorit Gupto
Language - Kiswahili
Level - First sentences