Anansi awapa watu hekima
Ghanaian folktale
Wiehan de Jager

Hapo zamani za kale, watu hawakujua chochote. Hawakujua kupanda mimea, kushona nguo, wala kuuunda vyombo vya chuma.

Lakini mungu wa hekima, aliimiliki hekima yote ambayo watu walihitaji.

Alihifadhi hekima hiyo kwenye chungu cha udongo.

1

Siku moja, mungu wa hekima aliamua kumpa Buibui Anansi chungu hicho kilichojaa ujuzi na hekima.

Buibui Anansi alikitazama chungu kile. Na kila alipokitazama alipata kujua jambo jipya.

Alifuarahi sana.

2

Buibui Anansi alisema, "Nitakificha chungu hiki juu ya mti mrefu ili mtu mwingine asikifikie. Ningetaka kufaidika peke yangu."

Buibui Anansi alitengeneza kamba akaifungia kwenye chungu. Alijifungia kamba hiyo kiunoni. Aliukwea mti chungu kikining'inia mbele yake.

Haikuwa rahisi kwani chungu kile kilimgonga magotini.

3

Wakati huo wote, mwanawe Buibui Anansi alikuwa amesimama chini ya ule mti akimtazama babake. Hatimaye, alimwuliza, "Baba, mbona usikifunge chungu mgongoni ili uweze kuuparaga mti?"

Anansi aliamua kukifunga mgongoni chungu hicho kilichojaa hekima. Ilikuwa rahisi zaidi kukibeba kile chungu mgongoni.

4

Baada ya muda mfupi, alifika juu ya mti.

Akiwa juu aliwaza, "Mimi ndiye ninabeba hekima lakini, mwanangu anaonekana kuwa mwerevu kuniliko."

Buibui Anansi alikasirika na kukitupa chini kile chungu.

5

Chungu kilianguka na kuvunjika vigae vingi.

Watu waliipata hekima wakajua kulima, kushona nguo, na kuunda vyombo vya chuma.

Hivyo ndivyo watu walijua kufanya mambo yote wanayofanya.

6
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Anansi awapa watu hekima
Author - Ghanaian folktale
Translation - Mutugi Kamundi
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - Longer paragraphs