Umoja
Ursula Nafula
Vusi Malindi

Kijiji chetu kilikuwa na shida nyingi. Tulikuwa na mfereji mmoja.

1

Tulitegemea chakula cha msaada.

2

Tuliogopa kuvamiwa na wezi.

3

Wazazi wengine hawakuweza kulipa karo.

4

Wasichana wadogo waliacha shule.

5

Wavulana wadogo walirandaranda kijijini.

6

Uchafu ulikuwa kila mahali.

7

Watu walikatwa na vipande vya chupa.

8

Siku moja, mfereji ulikosa maji.

9

Babangu aliwaita watu waende mkutano.

10

Watu walikusanyika wakajadiliana.

11

Babangu alisema, "Lazima tuyabadilishe maisha yetu."

12

Mimi nilisema, "Nitasafisha uwanja wa nyumba yetu."

13

Mamake Dama alisema, "Wanawake wataungana wapande chakula."

14

Babake Mumo alisema, "Wanaume watachimba kisima cha maji."

15

Kwa sauti moja tulisema, "Tuyabadilishe maisha yetu."

16
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Umoja
Author - Ursula Nafula
Adaptation - Ursula Nafula
Illustration - Vusi Malindi
Language - Kiswahili
Level - First words