Kuku amfanyia Tai hila
Nathan Higenyi
Rob Owen

Hapo zamani, Kuku na Tai walikuwa marafiki. Siku moja, Tai alimkuta Kuku akiwa anapumzika chini ya mti. Alikuwa amesimamia mguu mmoja pekee.

1

Tai alimwuliza Kuku, "Mguu wako mwingine uko wapi?"

2

Kuku alimweleza Tai, "Mwenye duka aliukata na badala yake akanipatia vitu hivi."

3

Tai alimwuliza Kuku ikiwa yeye pia angeweza kufanya hivyo. Vilevile alitaka mfuko uliojaa vitu. Kuku alikubali.

4

Tai alimwendea mwenye duka akitaka aukate mguu wake mmoja na badala yake ampatie vitu vitamu. Mwenye duka alikubali akafanya hivyo.

5

Tai aliruka ruka kwa mguu mmoja akielekea nyumbani. Hata hivyo, alivifurahia vitu alivopewa na mwenye duka.

6

Tai alipofika nyumbani, alimkuta Kuku akiwa na miguu yake miwili.

7

Tai alikasirika sana akaanza kumfukuza Kuku. Lakini hakuweza kumshika. Hiyo ndiyo sababu Tai huwashambulia vifaranga wa Kuku kila mara. Anapomshika mmoja, yeye humla.

8
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Kuku amfanyia Tai hila
Author - Nathan Higenyi
Translation - Ursula Nafula
Illustration - Rob Owen
Language - Kiswahili
Level - First paragraphs