Watoto walioumbwa kwa nta
Southern African Folktale
Wiehan de Jager

Hapo zamani za kale, kulikuwa na familia moja iliyoishi kwa amani.

1

Heri, Amani na Musa waliwasaidia wazazi nyumbani na shambani.

2

Wazazi wao hawakuwaruhusu waende karibu na moto, wala kukaa juani.

3

Heri, Amani na Musa walifanya kazi zao zote usiku.

4

Hii ni kwa sababu watoto hao waliumbwa kwa nta.

5

Musa alitamani kwenda nje wakati wa mchana.

6

Siku moja tamaa ilimzidi. Nduguze, Heri na Amani, walimwonya asiende juani. Musa hakuwasikiza.

7

Joto lilipokuwa kali, Musa aliyeyuka.

8

Heri na Amani walihuzunika walipomwona Musa akiyeyuka.

9

Heri na Amani waliichukua nta iliyoyeyuka wakamtengeneza ndege.

10

Kisha walimweka ndege huyo juu ya mlima mrefu.

11

Jua lilipochomoza, ndege huyo alipeperuka akiimba kwa furaha.

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Watoto walioumbwa kwa nta
Author - Southern African Folktale
Translation - Mutugi Kamundi
Illustration - Wiehan de Jager
Language - Kiswahili
Level - First sentences