Wangari Maathai
Nicola Rijsdijk
Maya Marshak

Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Wangari.

1

Wangari alipanda mbegu katika bustani yao.

2

Jioni, Wangari alirudi nyumbani.

3

Wangari alipofikisha umri wa miaka saba, alienda shule.

4

Wangari alifanya vyema shuleni.

Alialikwa kwenda Marekani kuendeleza masomo yake.

5

Alisomea sayansi ya viumbe, hasa mimea.

6

Hakusahau nchi yake ya Kenya.

7

Wangari aliporudi, Kenya ilikuwa imebadilika.

Miti mingi ilikuwa imekatwa.

8

Wangari aliwafundisha wanawake kupanda miti.

Waliiuza na kupata pesa.

9

Ujumbe wa Wangari ulienea Afrika nzima.

10

Wangari alipewa Tuzo la Amani la Nobel.

11

Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kiafrika kutuzwa.

Alifariki mwaka 2011.

12

Maswali: 1. Wangari alianza shule alipokuwa na miaka mingapi? 2. Wangari alienda Marekani kufanya nini? 3. Aliporudi Kenya, alikuta mabadiliko gani? 4. Wangari alipewa tuzo lipi? 5. Wangari Maathai alikuwa maarufu sana kwa kupanda miti na kutunza mazingira. Je, wewe unataka kuwa maarufu kwa kuchangia nini duniani?

13
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Wangari Maathai
Author - Nicola Rijsdijk
Adaptation - Ursula Nafula, Monica Shank
Illustration - Maya Marshak
Language - Kiswahili
Level - First sentences