Wangari Maathai
Nicola Rijsdijk
Maya Marshak

Kulikuwa na msichana mdogo aliyeitwa Wangari.

1

Wangari alipanda mbegu katika bustani yao.

2

Jioni, Wangari alirudi nyumbani.

3

Wangari alipofikisha umri wa miaka saba, alienda shule.

4

Wangari alifanya vyema shuleni.

Alienda Marekani kuendeleza masomo yake.

5

Alisomea Sayansi ya viumbe, hasa mimea.

6

Hakusahau nchi yake ya Kenya.

7

Wangari aliporudi, Kenya ilikuwa tofauti.

Miti mingi ilikuwa imekatwa.

8

Wangari aliwafunza wanawake kupanda miti.

Waliiuza na kupata pesa.

9

Ujumbe wa Wangari ulienea Afrika nzima.

10

Wangari alipewa Tuzo la Amani la Nobel.

11

Alikuwa mwanamke wa kwanza wa Kiafrika kutuzwa.

Alifariki mwaka 2011.

12
You are free to download, copy, translate or adapt this story and use the illustrations as long as you attribute in the following way:
Wangari Maathai
Author - Nicola Rijsdijk
Adaptation - Ursula Nafula
Illustration - Maya Marshak
Language - Kiswahili
Level - First words